21Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote; mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa.
22Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu, au mnilipie fidia kutoka mali zenu,
23au niokoeni mikononi mwa adui, au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’?
24“Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya; nionyesheni nilikokosea.
25Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli! Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini?