4Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu, roho yangu inakunywa sumu yake; vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.
5Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani, au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula?
6Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi, au upo utamu katika ute mweupe wa yai?
7Ninakataa kuvigusa; vyakula vya aina hii hunichukiza.
8“Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,