6Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi, au upo utamu katika ute mweupe wa yai?
7Ninakataa kuvigusa; vyakula vya aina hii hunichukiza.
8“Laiti ningepata haja yangu, kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,
9kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda, kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!
10Ndipo bado ningekuwa na hii faraja, furaha yangu katika maumivu makali: kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.