Ayubu 7

Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena.

Job 7:9 (UKJV) As the cloud is consumed and vanishes away: so he that goes down to the grave shall come up no more.

7Kumbuka, Ee Mungu, maisha yangu ni kama pumzi; macho yangu kamwe hayataona tena raha.

8Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena; utanitafuta, wala sitakuwepo.

9Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena.

10Kamwe harudi tena nyumbani mwake; wala mahali pake hapatamjua tena.

11“Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.