Ayubu 7

Kamwe harudi tena nyumbani mwake; wala mahali pake hapatamjua tena.

Job 7:10 (UKJV) He shall return no more to his house, neither shall his place know him any more.

8Lile jicho linaloniona sasa halitaniona tena; utanitafuta, wala sitakuwepo.

9Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena.

10Kamwe harudi tena nyumbani mwake; wala mahali pake hapatamjua tena.

11“Kwa hiyo sitanyamaza; nitanena kutokana na maumivu makuu ya roho yangu, nitalalama kwa uchungu wa nafsi yangu.

12Je, mimi ni bahari, au mnyama mkubwa mno akaaye vilindini, hata uniweke chini ya ulinzi?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.