Ayubu 8

Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

Job 8:10 (UKJV) Shall not they teach you, and tell you, and utter words out of their heart?

8“Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini,

9kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.

10Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

11Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? Matete yaweza kustawi bila maji?

12Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, hunyauka haraka kuliko majani mengine.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.