13Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
14Lile analolitumainia huvunjika upesi; lile analolitegemea ni utando wa buibui.
15Huutegemea utando wake, lakini hausimami; huungʼangʼania, lakini haudumu.
16Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua, ukieneza machipukizi yake bustanini;
17huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, na kutafuta nafasi katikati ya mawe.