17huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, na kutafuta nafasi katikati ya mawe.
18Unapongʼolewa kutoka mahali pake, ndipo mahali pale huukana na kusema, ‘Mimi kamwe sikukuona.’
19Hakika uhai wake hunyauka, na kutoka udongoni mimea mingine huota.
20“Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia, wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.
21Bado atakijaza kinywa chako na kicheko, na midomo yako na kelele za shangwe.