9Yeye ndiye Muumba wa nyota za Dubu, na Orioni, Kilimia, na makundi ya nyota za kusini.
10Hutenda maajabu yasiyopimika, miujiza isiyoweza kuhesabiwa.
11Anapopita karibu nami, siwezi kumwona; apitapo mbele yangu, simtambui.
12Anapochukua kwa ghafula, ni nani awezaye kumzuia? Ni nani awezaye kumwambia, ‘Unafanya nini?’
13Mungu hataizuia hasira yake; hata jeshi kubwa la Rahabu lenye nguvu linajikunyata miguuni pake.