Ayubu 9

Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, kwa nini basi nitaabishwe bure?

Job 9:29 (UKJV) If I be wicked, why then labour I in vain?

27Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu, nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’

28bado ninahofia mateso yangu yote, kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.

29Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, kwa nini basi nitaabishwe bure?

30Hata kama ningejiosha kwa sabuni na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

31wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.