39Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.
40Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.
41“Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu.
42Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
43Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea.