40Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.
41“Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu.
42Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
43Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea.
44Ninyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu?