26Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.
27Koo za Walawi za Wagershoni walipewa: kutoka nusu ya kabila la Manase, Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;
28kutoka kabila la Isakari walipewa, Kishioni, Daberathi,
29Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne
30kutoka kabila la Asheri walipewa, Mishali, Abdoni,