Waamuzi 1

wale wapelelezi wakaona mtu anatoka mjini, nao wakamwambia, “Tuonyeshe jinsi ya kuingia mjini nasi tutakutendea wema.”

Judges 1:24 (UKJV) And the spies saw a man come forth out of the city, and they said unto him, Show us, we pray you, the entrance into the city, and we will show you mercy.

22Basi nyumba ya Yosefu wakashambulia Betheli, naye Bwana alikuwa pamoja nao.

23Walipotuma watu kwenda kupeleleza Betheli (ambao hapo kwanza uliitwa Luzu),

24wale wapelelezi wakaona mtu anatoka mjini, nao wakamwambia, “Tuonyeshe jinsi ya kuingia mjini nasi tutakutendea wema.”

25Hivyo akawaonyesha, nao wakaupiga mji kwa upanga lakini wakamhifadhi hai yule mtu na jamaa yake yote.

26Yule mtu akaenda hadi nchi ya Wahiti, ambapo aliujenga mji na kuuita Luzu, ambao ndio jina lake hadi leo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.