8Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
9Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani.
10Ngozi yetu ina joto kama tanuru, kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
11Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni, na mabikira katika miji ya Yuda.
12Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima.