12Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima.
13Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia, wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
14Wazee wameondoka langoni la mji, vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
15Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
16Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!