14Wazee wameondoka langoni la mji, vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
15Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
16Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
17Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
18kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, nao mbweha wanatembea juu yake.