67Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema:
68“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.
69Naye ametusimamishia pembe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi wake,
70kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani,
71kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao: