1Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini.
2Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi,
3lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu.
4Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayongʼaa kama umeme wakasimama karibu nao.