38pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.
39Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko.
40Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.
41Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.
42Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.