36Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu.
38Kwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri.
39Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
40Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.