1Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:
2Kwa kupata hekima na nidhamu; kwa kufahamu maneno ya busara;
3kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
4huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana;
5wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo;