3kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
4huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana;
5wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo;
6kwa kufahamu mithali na mifano, misemo na vitendawili vya wenye hekima.
7Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.