Mithali 10

Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.

Proverbs 10:12 (UKJV) Hatred stirs up strifes: but love covers all sins.

10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia.

11Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.

12Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.

13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.

14Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.