15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini.
16Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu.
17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.
18Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu.
19Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.