13Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.
14Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.
15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini.
16Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu.
17Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.