21Midomo ya mwenye haki hulisha wengi, lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu.
22Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni.
23Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.
24Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.
25Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.