25Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.
26Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
27Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
28Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.
29Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.