Mithali 10

Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.

Proverbs 10:3 (UKJV) The LORD will not suffer the soul of the righteous to famish: but he casts away the substance of the wicked.

1Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake.

2Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.

3Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.

4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.

5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.