2Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.
3Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.
4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.
5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.