29Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.
30Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi.
31Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa upotovu utakatwa.
32Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.