6Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.
7Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza.
8Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia.
9Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.
10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia.