Mithali 11

Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

Proverbs 11:18 (UKJV) The wicked works a deceitful work: but to him that sows righteousness shall be a sure reward.

16Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima, bali wanaume wakorofi hupata mali tu.

17Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe, bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.

18Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

19Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.

20Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu, bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.