9Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.
10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake.
11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi.
12Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.