11Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi.
12Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
13Hata katika kicheko moyo waweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
14Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao, naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake.
15Mtu mjinga huamini kila kitu, bali mwenye busara hufikiria hatua zake.