23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.
24Utajiri wa wenye hekima ni taji yao, bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.
25Shahidi wa kweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.
26Yeye amchaye Bwana ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.
27Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.