6Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya waovu huwaletea taabu.
7Midomo ya mwenye hekima hueneza maarifa, bali sivyo ilivyo mioyo ya wapumbavu.
8Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu humfurahisha Mungu.
9Bwana huchukia sana njia ya waovu, bali huwapenda wale wafuatao haki.
10Adhabu kali humngoja yeye aachaye njia; yeye achukiaye maonyo atakufa.