8Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.
10Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki.
11Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Bwana; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye.
12Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki.