6Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.
7Njia za mtu zinapompendeza Bwana, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.
8Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.
10Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki.