16Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha!
17Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.
18Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko.
19Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.
20Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Bwana.