1Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.
2Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Bwana.
3Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.
4Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi.
5Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.