30Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.
31Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu.
32Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
33Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.