18Kupiga kura hukomesha mashindano na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika kuliko mji uliozungushiwa ngome, nayo mabishano ni kama malango ya ngome yenye makomeo.
20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake, atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.
22Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana.