20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake, atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, nao waupendao watakula matunda yake.
22Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa Bwana.
23Mtu maskini huomba kuhurumiwa bali tajiri hujibu kwa ukali.
24Mtu mwenye marafiki wengi wanaweza kumharibu, bali yuko rafiki aambatanaye na mtu kwa karibu kuliko ndugu.