10Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Bwana huchukia vyote viwili.
11Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili.
12Masikio yasikiayo na macho yaonayo, Bwana ndiye alivifanya vyote viwili.
13Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.