24Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.
25Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.
26Mchana kutwa hutamani zaidi, lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.
27Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo, si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya!
28Shahidi wa uongo ataangamia, bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.