14Mwadhibu kwa fimbo na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini.
15Mwanangu, kama moyo wako una hekima, basi moyo wangu utafurahi,
16utu wangu wa ndani utafurahi, wakati midomo yako itakapozungumza lililo sawa.
17Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.
18Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.