20kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa.
21Mwanangu, mche Bwana na mfalme, wala usijiunge na waasi,
22kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?
23Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema:
24Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” Kabila zitamlaani na mataifa yatamkana.