15Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua.
16Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.
17Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
18Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.
19Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.