23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako.
24Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote.
25Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa,
26wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba.
27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike.